Uturuki
Uturuki ni nchi yenye historia ndefu na tajiri inayochanganya utamaduni wa Asia na Ulaya. Katika historia yake, eneo hili lilikuwa kitovu cha milki kubwa kama vile Ufalme wa Bizanti na baadaye Milki ya Osmani (Ottoman Empire) ambayo ilidumu kwa zaidi ya miaka 600 hadi kuvunjwa kwake mwaka 1922. Jamhuri ya Uturuki ilitangazwa rasmi tarehe 29 Oktoba 1923 chini ya uongozi wa Mustafa Kemal Atatürk, ambaye alianzisha mageuzi makubwa ya kisiasa, kijamii, na kiuchumi yaliyolenga kuifanya Uturuki kuwa taifa la kisasa na la kidemokrasia. Leo, Uturuki ni jamhuri ya urais yenye maendeleo ya kati hadi ya juu kiuchumi, ikiwa mwanachama wa mashirika mbalimbali ya kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa, G20, NATO, na Shirika la Ushirikiano wa Kiislamu (OIC). Uchumi wake unaegemea kwenye viwanda, kilimo, utalii, na huduma, huku miji mikuu kama Istanbul, [[Ankara[], na Izmir ikiwa vituo vikuu vya biashara na utamaduni. Licha ya maendeleo haya, nchi imekabiliwa pia na changamoto za kisiasa, kijamii, na kiusalama, hasa kutokana na migogoro ya kikanda na masuala ya ndani ya kisiasa. Jiografia![]() Sehemu kubwa ya mipaka yake ni bahari: Mediteranea upande wa magharibi na kusini na Bahari Nyeusi upande wa kaskazini. Kwenye nchi kavu imepakana na Ugiriki na Bulgaria upande wa magharibi, Kaskazini-mashariki na Georgia, Armenia na Azerbaijan, kwa upande wa mashariki na Iran na upande wa kusini na Iraq na Syria. Sehemu kubwa ya eneo lake ni Anatolia inayoonekana kama rasi kubwa kati ya Mediteranea na Bahari Nyeusi. Hali ya nchi ndani ya Anatolia mara nyingi ni yabisi na kilimo kinategemea umwagiliaji. Safu za milima zinafuatana na pwani za kusini na kaskazini. Sehemu ya mashariki ya nchi kuelekea Uajemi na Kaukazi ina milima mingi. Maeneo ya pwani yanapokea mvua na huwa na rutuba. HistoriaWaturuki waliwahi kuwa kiini cha Milki ya Osmani iliyounganisha mataifa mengi chini ya Sultani wa Konstantinopoli. Uturuki wa kisasa umetokea kama nchi ya pekee baada ya vita viwili mwanzoni mwa karne ya 20. Jamhuri ya Uturuki ilianzishwa mwaka 1923 na jenerali Kemal Atatürk baada ya vita vikuu vya kwanza, vilivyomalizika kwa kuvunja Milki ya Osmani, na vita vilivyofuata, vya kuondoa wanajeshi wa Ugiriki na nchi nyingine walioingia ndani ya sehemu iliyokuwa imebaki baada ya kuvunjika kwa dola kubwa. Atatürk alileta mabadiliko mengi yaliyolenga kuondoa utamaduni wa kale wa Waosmani na enzi za utawala wa sultani wa Kiislamu. Magharibi ya nchi imeendelea sana lakini maeneo ya mashariki yamebaki nyuma. Nchi ya kisasaSiku hizi Uturuki unalenga kuingia katika Umoja wa Ulaya. Serikali ina utaratibu wa kidemokrasia ya vyama vingi. Utawala wa nchi ni kwa mikoa 81. Mji mkuu ni Ankara ulioko katika kitovu cha Anatolia. Mji mkubwa ni Istanbul ulioitwa zamani Konstantinopoli na zamani zaidi Bizanti: ulikuwa mji mkuu wa Dola la Uturuki hadi mwaka 1923. DemografiaUturuki una wakazi zaidi ya milioni 76. Wengi wao (70-75%) ni Waturuki. Katika mashariki ya Uturuki watu wengi ni Wakurdi ambao ni milioni 14 au takriban 20% za raia wote wa Uturuki.[1] Kuna mabaki madogo tu ya Wagiriki na Waarmenia waliowahi kukalia sehemu kubwa za nchi hadi mwisho wa milki ya Osmani. Kwenye maeneo jirani na Syria wako pia Waarabu. Lugha rasmi na ya kawaida ni Kituruki, kinachotimika na 85% za wakazi. Hata hivyo, lugha 36 huzungumzwa nchini Uturuki, yaani 14 za asili na 22 za nje (angalia orodha ya lugha za Uturuki). Upande wa dini, karibu wote ni Waislamu, hasa kuanzia karne ya 20 ambapo Wakristo wengi waliuawa (hasa Waarmenia) au kuhama (hasa Wagiriki). Waliobaki ni 0.2% tu. Hata hivyo Uturuki ni nchi isiyo na dini rasmi. Picha za Uturuki
Tazama piaViungo vya nje
|