Bahrain
![]() ![]() Bahrain (kwa Kiarabu: مملكة البحرين Mamlakat al-Baḥrayn, Ufalme wa Bahrain) ni nchi ya visiwa na ufalme mdogo katika Ghuba ya Uajemi karibu na pwani ya Saudi Arabia. Nchi ni tajiri kutokana na mapato ya mafuta ya petroli. JiografiaBahrain iko upande wa mashariki wa Bara Arabu. Eneo lake lina visiwa asilia 50 na vingine 33 vilivyotengenezwa na binadamu. Vikubwa kati ya hivyo ni:
Nchi ni tambarare; kilima cha juu ni Jabal ad-Dukhan chenye m 137 juu ya UB. Sehemu kubwa ya eneo ni jangwa, lakini kaskazini mwa kisiwa kikuu pana visima na kilimo cha bustani na mitende. HistoriaBahrain ndiyo makao ya ustaarabu wa Dilmun. Ilipata umaarufu tangu zamani kwa kuvua lulu bora kuliko zote duniani hadi karne ya 19. Bahrain ilikuwa kati ya maeneo ya kwanza kuongokea Uislamu, mwaka 628 BK. Baada ya kipindi cha utawala wa Waarabu, Bahrain ilitekwa na Wareno mwaka 1521 hadi 1602 walipofukuzwa na Shah Abbas I wa nasaba ya Safavid chini ya Dola la Uajemi. Mwaka 1783, ukoo wa Bani Utbah uliteka Bahrain kutoka kwa Nasr Al-Madhkur na tangu hapo nchi imetawaliwa na ukoo wa Al Khalifa, Ahmed al Fateh akiwa hakimu wa kwanza wa Bahrain. Tangu mwaka 1820 Visiwa hivyo pamoja na Qatar na Falme za Kiarabu vilikuwa na mikataba na Uingereza walipoahidi kuachana na uharamia na kupokea ulinzi wa Uingereza. Ulinzi huo ulizuia uvamizi wa Saudia katika karne ya 20. Falme hizo zilikuwa nchi lindwa chini ya Uingereza hadi mwaka 1971, ambapo madola hayo madogo yalipata uhuru. WakaziWakazi wengi (54%) ni wahamiaji kutoka nchi nyingi duniani, hasa India na nchi nyingine za Asia (43.4%), wakiwa na lugha na dini mbalimbali. Wenyeji (46%) ni Waarabu, lakini pia Waajemi, Wabeluchi na Waafrika. Lugha rasmi ni Kiarabu, lakini baadhi ya wenyeji na wahamiaji wengi wanatumia kwanza lugha nyingine. Kiingereza kina nafasi kubwa. Upande wa dini, wengi (80.6%) ni Waislamu, ila upande wa madhehebu wamegawanyika kati ya Washia (65-75%) na Wasuni. Uislamu ndio dini rasmi. Wakristo wa madhehebu mbalimbali ni asilimia 12.1, wakiwemo wahamiaji wengi, lakini pia wenyeji. Wahindu ni 6.4% na Wabuddha 0.4%. UchumiUchumi wa Bahrain hutegemea hasa mafuta ya petroli yanayozalisha 30% ya pato la taifa na 60% za mapato yote ya serikali. Serikali imejitahidi kujenga matawi mengine ya uchumi hasa viwanda vinavyotumia mafuta kwa kutengeneza bidhaa za aina nyingi pamoja na biashara. Kati ya nchi za Kiarabu ndiyo inayostawi kiuchumi haraka zaidi. Tazama piaViungo vya nje
|