Myanmar
Imepakana na China upande wa kaskazini, Laos upande wa mashariki, Uthai kusini-mashariki, Bangladesh na Uhindi magharibi. Kuna pwani kwenye Bahari Hindi yenye urefu wa km 2,000. JiografiaKaskazini mwa nchi kuna milima mingi. Safu tatu za Rakhine Yoma, Bago Yoma na Nyanda za Juu za Shan zimeanza katika Himalaya na kuelekea kusini. Milima ya Hengduan Shan iko mpakani kwa China. Mlima mkubwa ni Hkakabo Razi kwenye jimbo la Kachin wenye kimo cha mita 5,881. Mito mitatu mikubwa ya Myanmar inavuka kati ya safu za milima; niː Mto Ayeyarwady ni mto mkubwa wa Myanmar wenye urefu wa km 2,170. Bonde lake ni la rutuba na lina wakazi wengi. Karibu nusu ya nchi imefunikwa na misitu. Miji mikubkwa
HistoriaTangu karne ya 9 BK nchi iliona falme mbalimbali zilizotawala kutoka mji mkuu wa Pagan. Katika karne ya 19 Uingereza ulianza kujishughulisha na habari za Burma (Myanmar) baada ya kutawala maeneo jirani ya Uhindi. Kwa vita tatu kati ya miaka 1826 na 1885 Uingereza ulieneza utawala wake. Burma ilikuwa sehemu ya Uhindi wa Kiingereza tangu 1885. Mwaka 1937 Waingereza walianza kutawala Burma kama koloni la pekee. Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia Japan ilitwaa karibu nchi yote. Baada ya vita Burma ikapata uhuru wake tarehe 4 Januari 1948. Serikali iliyochaguliwa kidemokrasia ilipinduliwa na jeshi mwaka 1962. Mtawala mpya hadi mwaka 1988 alikuwa jenerali Ne Win aliyetangaza siasa ya "Ujamaa wa Kiburma". Upinzani ulikandamizwa vikali mara kadhaa. Nchi iliona harakati kwa ajili ya demokrasia na dhidi ya udikteta mwaka 1988; hapo Ne Win alijiuzulu. Baada ya maandamano yaliyokandamizwa mara kadhaa, Jenerali Saw Maung alichukua utawala kwa nguvu ya kijeshi. Uchaguzi huru wa mwaka 1989 ulileta ushindi wa chama cha NLD, chini ya Aung San Suu Kyi, lakini kamati ya kijeshi ilikataa kukabidhi madaraka. Burma ilibadilishiwa jina kuitwa "Myanmar" ikaendelea kutawaliwa na serikali ya kijeshi hadi mwaka 2011. Upinzani haukuruhusiwa. UtawalaMyanmar imegawiwa kwa kusudi la utawala katika madola 7 na mikoa 7. "Madola" ni maeneo yanayokaliwa na jumuiya na makabila ambayo ni tofauti na kundi kubwa la taifa linaloitwa Bamar. Maeneo ya Bamar huitwa mikoa. ![]() Madola ya jumuiya ndogo yapo zaidi karibu na mipaka ya nchi. Kuanzia kusini-magharibi ni haya yafuatayo:
Halafu kuna mikoa 7:
Mazingira ya mji mkuu Naypyidaw ni eneo la kitaifa la Naypyidaw. Madola na mikoa imegawiwa katika wilaya, tarafa, kata na vijiji. WatuMyanmar ni nchi ya makabila mengi (135 yametambulika rasmi) na lugha nyingi (angalia orodha ya lugha za Myanmar). Kundi kubwa (68%) ni Waburma wenye asili katika milima ya Tibet walikotokea mababu wao miaka 1000 hivi iliyopita. Lugha kubwa ni Kiburma, ambacho ndicho lugha rasmi. Wakazi walio wengi (80%) hufuata dini ya Ubuddha, hasa ya madhehebu ya Theravada. Wakristo ni 7%, wafuasi wa dini za jadi ni 6%, Waislamu ni 4%, Wahindu ni 2%. PichaTazama piaViungo vya nje
|