Niyasov alibadilisha utawala wa chama cha kikomunisti kuwa udikteta wake mwenyewe. Akaanza kutumia jina la "Turkmenbashi" (Baba wa Waturkmeni wote) na sanamu zake zikasimamishwa kote nchiniː mara nyingi zilikuwa sanamu za dhahabu hata kama wananchi walikuwa na maisha magumu.
Mapato kutoka gesi na mafuta ya petroli yalimwezesha kuendesha uchumi wa nchi kwa hiari yake bila mabadiliko makubwa jinsi ilivyokuwa kawaida wakati wa anguko la ukomunisti kwingineko.
Zaidi ya nusu ya wananchi walikuwa hawana ajira na kuishi maisha ya umaskini, lakini wanapewa chumvi, umeme na maji bure. Mkate na petroli zinauzwa kwa bei ya chini sana, lakini kuna uhaba wa mara kwa mara.
Mwenyekiti wa bunge alishtakiwa mahakamani juu ya makosa fulani na Berdimuhammedov alithibitishwa katika uchaguzi wa tarehe11 Februari2007 kwa 89% za kura. Watazamaji walidai kura ilikuwa ya uwongo.
Mwaka 2013 kwa mara ya kwanza ulifanyika uchaguzi wa vyama vingi.
Watu
Waturkmeni wenyewe ni 81.8% za wakazi wote, wakifuatwa na Wauzbeki (9.4%), Warusi (2.2%), Wakazaki (1.6%) na Waarmenia (1.1%).
Wakazi walio wengi ni Waislamu; kuna kadirio ya Waislamu asilimia 96.1 kati ya wakazi wote lakini haijulikani ni wangapi wanaofuata kweli dini yao. Wakristo ni 3.6%, hasa Waorthodoksi.
1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Turkmenistan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.