Baba![]() Baba ni mwanamume aliyemzaa mtoto au anamlea. Katika uzazi, baba ndiye anayesababisha jinsia ya mtoto kwa kumrithisha chembeuzi Y (mtoto wa kiume) au chembeuzi X tu (mtoto wa kike). Saikolojia inaonyesha pia umuhimu wa kuwepo kwa baba mwenye pendo, akishirikiana na mama, katika kukua kwa mtoto. Kujiandaa kuwa baba boraKugundua kuwa utakuwa baba hivi karibuni inafurahisha sana, haswa ikiwa ni mara yako ya kwanza kuwa baba. Kuwa baba ni jukumu la kipekee sana na muda mwingine unaweza kuhisi furaha na woga vyote kwa wakati mmoja. Ingawa unaweza usijisikie kamwe uko “tayari” kabisa kuwa baba, kuna hatua unazoweza kuchukua ili kujitayarisha kiakili na kihisia kama vile:- Kufanya utafiti wako, kuhusika kikamilifu katika ujauzito, na kuamua kimakusudi ni aina gani ya baba unayetaka kuwa kunaweza kukusaidia kuwa tayari zaidi kwa ajili ya kuwa baba[1]. Tafuta taarifa sahihiAkina baba wengi hawajui nini cha kufanya linapokuja suala la uzazi na mara nyingi huogopa mtoto akishazalia ni vitu gani vya msingi anatakiwa afanye kama baba.1 Ikiwa unahisi kupotea kidogo, inaweza kusaidia kufanya utafiti wako kuhusu ujauzito na uzazi[2]. Iwe unapenda kusoma vitabu, kusikiliza podikasti, kutazama video, kuonana na wataalamu kwaajili ya ushauri au kuhudhuria mafunzo mbalimbali, yote hayo yana maelezo mengi na taarifa muhimu muhimu kuhusu wazazi wanaotarajia kupata mtoto hivi karibuni[3]. Shiriki kikamilifu katika muda wote wa ujauzitoSafari yako kama baba huanza mapema kabla mtoto wako hajazaliwa. vitu kama vile Kuthibitisha ujauzito na muda wake, kuona fetusi kwenye uchunguzi wa ultrasound, na kusikia mapigo ya moyo wake kwa mara ya kwanza ni baadhi ya hatua kuu za kushiriki kikamilifu kwa wakati huu. Kushiriki kikamilifu katika ujauzito kunaweza kukusaidia kufurahia vitu ambavyo hukufifahamu mwanzo, kuungana na mpenzi wako, na kumsaidia kupitia mchakato huo[4]. Hizi ni baadhi ya njia unazoweza kushiriki kikamilifu kipindi cha ujauzito[5]:
Tanbihi
Viungo vya nje
|