Inaweza kutengenezwa kwa kuchonga au kwa njia nyingine (k.mf. kumimina kiowevu katika muundo uliokusudiwa).
Historia
Sanamu zilitengenezwa tangu zamani za historia ya awali (walau miaka 30,000 hivi iliyopita) na katika utamaduni mbalimbali wa dunia nzima. Ile ndefu zaidi ni sanamu ya Buddha inayopatikana China ikiwa na urefu wa mita 128.
Mara nyingi sanamu inaagizwa kama kumbukumbu ya tukio fulani au mtu maarufu na inawekwa mahali pa hadhara.
Katika dini
Dini mbalimbali, hasa Uyahudi na Uislamu, zimekataza sanamu na picha zote.
Katika Ukristo suala lilijadiliwa kwa nguvu zote hasa katika karne ya 7 na ya 8 likamalizika katika mtaguso wa pili wa Nisea. Hata hivyo, baadaye lilizuka tena na tena, hivi kwamba msimamo wa madhehebu ni tofauti sana.
Picha
Simba-mtu, Hohlenstein-Stadel, Ujerumani, sasa katika Ulmer Museum, Ulm, ni sanamu ya kale kuliko zote zinazojulikana kuonyesha kiumbehai, 40,000 - 30,000 KK
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Sanamu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.