Waarabu (kwa Kiarabu عَرَبِ, matamshi ya Kiarabu: [ʕarabi]) ni watu ambao lugha mama yao ni Kiarabu wakijitambua vile.
Asili ya Waarabu na uenezaji
Kiasili walikuwa watu wa Bara Arabu na maeneo jirani katika Syria na Iraki[1], lakini tangu kuja kwa Uislamu walienea nje ya eneo asilia hasa katika Afrika ya Kaskazini na nchi za Mashariki ya Kati ambako walijichangaya na wenyeji ambao wengi wao wamepokea lugha ya Kiarabu tangu karne nyingi na kujitazama kama Waarabu pia.
Dini ya Uislamu ilianzia kati ya Waarabu na hivyo Kiarabu ndiyo lugha ya Qurani na maandiko ya Kiislamu, na Waarabu wengi ni Waislamu. Walakini kati ya Waislamu wote Waarabu ni kama asilimia 20 tu. [7]
Baada ya Muhamad, makhalifa wa kwanza (632-661 BK) waliunganisha Waarabu wote chini ya utawala wao wakaendelea kuvamia milki jirani za Dola la Roma na Uajemi ya Wasasani. ote walianza kutumia lugha ya Kiarabu kama lugha ya utawala. Makabila mengi kutoka Bara Arabu yalianza kuhamia nchi zilizovamiwa katika hiyo milki kubwa ya Kiislamu iliyoenea kutoka Moroko na Hispania upande wa magharibi hadi mipaka ya China na Uhindi upande wa mashariki.[9] Katika karne zilofuata, wakazi wengi wa maeneo hayo walianza kuwa Waislamu na kutumia Kiarabu kama lugha ya kidini na ya kielimu; hasa katika sehemu kubwa ya Afrika Kaskazini pamoja na Misri na katika nchi za Asia Magharibi (hasa nchi za leo Syria, Lebanoni, Iraki) wenyeji wengi walianza kutumia Kiarabu kama lugha yao na hivyo kuitwa Waarabu.
Wakati wa kuzaliwa kwa Mtume Muhamad lugha ya Kiarabu ilitumika Uarabuni tu, nchi ya jangwa na oasisi. Kutoka hapa makabila ya Waarabu Waislamu walivamia nchi jirani ambako wenyeji walitumia lugha mbalimbali. Lugha kadhaa zimeendelea kwa viwango vidogo, vingine vimebaki na nguvu zaidi. Lugha ya Kiaramu iliyowahi kutamalaki katika siasa na uchumi kuanzia Syria hadi Uajemi na zaidi, imebaki kati watu wa vijiji katika maeneo ya kaskazini ya Syria na Iraki, pia kama lugha ya liturgia kanisani. Kikopti iliyokuwa lugha ya Misri imebaki pekee katika liturgia ya kanisa ilhali Wakristo Wakopti wanaongea Kiarabu tu. Kiberber bado inazungumzwa na milioni kadhaa katika Moroko na Algeria. Kikurdi ina nguvu katika milima ya Syria na Iraki kaskazini. Kiajemi (lugha ya Iran) kimefaulu kurudi kama lugha ya kitaifa lakini imepokea karibu asilimia 40 za msamiati wake kutoka Kiarabu; atahri kubwa ya lugha ya Kiarabu inaonekana pia katika lugha nyingine nyingi hadi Kiswahili.
Katika nchi zinazoitwa Kiarabu, lugha ya Kiarabu imekuwa lugha ya kila siku ya kuongea na pia ya serikali, biashara na utamaduni hata kwa hao ambao bado wmetunza lugha nyingine kama lugha yao ya kwanza[13].
Dini
Kwa upande wa dini, Waarabu huwa na tofauti kati yao.
Katika zama za kabla ya Uislamu, Waarabu wengi walifuata dini za kuabudu miungu mingi. Makabila kadhaa yalikuwa yamekubali Ukristo au Uyahudi na watu wachache waliotwa hanif walisemekana kuwa na imani kwa Mungu mmoja. [14]
Leo, karibu asilimia 93 za Waarabu ni wafuasi wa Uislamu[15]. Kuna pia Wakristo kama jumuiya ndogo zaidi. [16] Waislamu Waarabu kimsingi ni wa madhehebu ya Wasunni, Washiia, Waibadi na Waalawi.
Wakristo wa Kiarabu kwa ujumla hufuata moja ya Makanisa ya Kikristo ya Mashariki, kama yale yaliyo ndani ya makanisa ya Orthodox yaMashariki, makanisa Katoliki ya Mashariki, au makanisa ya Kiprotestanti ya Mashariki. [17] Kuna pia idadi ndogo ya Wayahudi wa Kiarabu ambao bado wanaishi katika nchi za Kiarabu lakini wengi wao waliondoka kwao wakihamia Israeli au nchi nyingine za Ulaya na Amerika. Sehemu ya Wakristo katika nchi za Kiarabu hawajitambui kuwa Waarabu kwa mfano Wakopti au Waashuri.
↑Bureš, Jaroslav (2008). Main characteristic and development trends of migration in the Arab world. Prague: Institute of International Relations. ISBN978-80-86506-71-5.
↑"Arab (People)". Britannica. Iliwekwa mnamo 19 Desemba 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
↑Bureš, Jaroslav (2008). Main characteristic and development trends of migration in the Arab world. Prague: Institute of International Relations. ISBN978-8086506715.
↑Chapter 4. Modern Standard Arabs". Nationalism, Language, and Muslim Exceptionalism, Philadelphia: University of Pennsylvania Press, 2015, pp. 53-85. https://doi.org/10.9783/9780812291018.53
↑"Demographics of Islam". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 9 Oktoba 2020. Iliwekwa mnamo 28 Septemba 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
↑Ruthven, Albert Hourani; with a new afterword by Malise (2010). A history of the Arab peoples (tol. la 1st Harvard Press pbk.). Cambridge, Mass.: Belknap Press of Harvard University Press. ISBN978-0-674-05819-4.{{cite book}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
↑Rogan, Eugene L. (2004). Frontiers of the state in the late Ottoman Empire : Transjordan, 1850–1921. Cambridge University Press. ISBN978-0-521-89223-0. OCLC826413749.
↑Bernard Ellis Lewis; Buntzie Ellis Churchill (2008). Islam: The Religion and the People. Pearson Prentice Hall. uk. 137. Iliwekwa mnamo 21 Agosti 2017. At the time of the Prophet's birth and mission, the Arabic language was more or less confined to Arabia, a land of deserts, sprinkled with oases. Surrounding it on land on every side were the two rival empires of Persia and Byzantium. The countries of what now make up the Arab world were divided between the two of them—Iraq under Persian rule, Syria, Palestine, and North Africa part of the Byzantine Empire. They spoke a variety of different languages and were for the most part Christians, with some Jewish minorities. Their Arabization and Islamization took place with the vast expansion of Islam in the decades and centuries following the death of the Prophet in 632 CE. The Aramaic language, once dominant in the Fertile Crescent, survives in only a few remote villages and in the rituals of the Eastern churches. Coptic, the language of Christian Egypt before the Arab conquest, has been entirely replaced by Arabic except in the church liturgy. Some earlier languages have survived, notably Kurdish in Southwest Asia and Berber in North Africa, but Arabic, in one form or another, has in effect become the language of everyday speech as well as of government, commerce and culture in what has come to be known as "the Arab world."{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)