Bab![]() ![]() Bab (kwa Kiarabu: الباب al-bab, wa maana ya "Geti la Mungu"; 20. Oktoba 1819 huko Shiraz, Iran; 9. Julai 1850 huko Tabriz, Iran) ni jina la heshima la kidini la Sayyid ʿAli Muhammad Shirazi (kwa Kifarsi: سيد علی محمد شیرازی ) aliyekuwa mwanzilishi wa dini ya Ubabi. Wababi na Wabahai wanaamini alikuwa Mdhihirishaji wa Mungu. FamiliaBaba wa Sayyid Ali Muhammad alikuwa mfanyabiashara mashuhuri mjini Shiraz, alifariki muda mfupi baada ya kuzaliwa kwake, kwa hiyo alilelewa na mjomba Haji Mirza Sayyid Ali, mfanyabiashara pia. Alipofikia umri wa kukomaa, alijiunga na biashara ya familia akishirikiana na mjomba wake. Alitambuliwa na wenzake kuwa mtu mwaminifu aliyeonyesha ukarimu kwa wale walio na uhitaji. Hakufurahia sana na biashara akipendelea kusoma vitabu vya dini ma kutumia muda mwingi katika sala. Mjomba alimtuma Bushehr iliyokuwa wakati ule bandari kubwa ya Uajemi kwenye Ghuba ya Uajemi. Mwaka 1842 alimwoa Khadíjih-Bagum akazaa naye mtoto mmoja aliyeitwa Aḥmad lakini alifariki mapema. Mazingira ya kidiniWakati ule kulikuwa na harakati ya "Washeikhi" waliokuwa wafuasi wa Sheikh Ahmad aliyehubiri kurudi kwa Imamu wa 12 aliye Mahdi wa Washia kulikuwa karibu sana. Kiongozi wa pili baada ya Sheikh Ahmad alikuwa Kazim Rashti (1793–1843) aliyewaambia wafuasi wake kuwa Mahdi ameshafika tayari, aliwatuma waende wamtafute. Mmoja wa wafuasi hao alikuwa Mulla Husain aliyesafiri katika miji mingi ya Uajemi (Iran) akimtafuta Mahdi. UfunuoKatika Mei 1844 Mulla Husein alifika Shiraz ambapo alikutana na Ali Muhammad aliyemkaribisha nyumbani kwake. Wakati wa mazungumzo, Husein alimueleza mwenyeji wake kusudi la safari yake na nani alimtafuta, mwenyeji wake alimjibu ni yeye aliyemtafuta. Usiku ule akiwa mjini Shiraz, Sayyid Ali Muhammad aliandika kwa kasi kubwa mlango wa kwanza wa kitabu chake cha tafsir ya sura 12 ya Kurani huku Mulla Husain na mke wake wakimtazama. Kuanzia usiku ule alijiita Bab, alidai kuwa ni mdomo wa Mungu ulioahidiwa na manabii wa siku za zamani akiwa yeye mlango au geti linalounganisha waumini na Mahdi anayetarijiwa. Mulla Husain alikuwa mwumini wa kwanza aliyekubali ufunuo huo. Herufi za uhaiBaada ya Mulla Husain kumkubali Bab, Bab alimwambia asubiri kabla ya kuhubiri hadi wafuasi 17 wengine watakapokuwa wamefika kwake. Katika muda mfupi, waumini wengine 17 walimtambua "kwa utafutaji wao wenyewe". Kati ya wanafunzi hao 18 alikuwepo pia mwanamke mmoja, Zarrin Tāj Baraghāni, aliyekuwa mashuhuri kama mshairi kwa jina la Qurrat al-ʿAyn (kwa Kiarabu: "faraja ya macho") au kama Ṭāhira (kwa Kiarabu: "safi"), na baadaye aliitwa mwanaharakati wa kwanza wa haki za wanawake huko Mashariki ya Kati. Bab aliwaita wanafunzi hao 18 "Herufi Hai" akawatuma kwenda sehemu mbalimbali za Uajemi na Turkestan ili kueneza habari ya kuwasili kwake. Hija ya kwenda Makka na MadinaBab mwenyewe alikwenda Hija huko Makka na Madina mnamo Novemba 1844 na "Herufi Hai" Quddus, ambapo alitangaza utume wake wazi. Aliandika barua kwa Sharifu wa Makka akajitangaza kuwa Imamu wa 12. Kukamatwa na Kufukuza![]() Baada ya kurudi Iran, viongozi wa Uislamu walianza kumstaki na kuhubiri dhidi yake. Bab alikamatwa mara ya kwanza Shiraz, baadaye Isfahan. Kutoka kule alitumwa kama mfungwa Teheran na baadaye Tabriz. Gereza na mauti![]() Katika msimu wa joto wa 1847, Bab alihamishwa kwenye ngome ya mlima wa Maku, magharibi mwa Azerbaijan alipofungwa siku 40. Mnamo Julai 1848 alipelekwa huko Tabriz, ambapo alihojiwa na mahakama ya wataalamu wa Uislamu. Walipendekeza kumpa adhabu ya kifo, lakini serikali, ilipendelea alikuwa na wafuasi wengi waliompenda, ilijaribu kumtangaza kichaa. Bab alipigwa vibaya akafungwa tena katika ngome. Mwaka 1850 waziri mkuu mpya Amir Kabir aliamua kumaliza kesi hiyo akaamuru kumuua. Tarehe 9 Julai 1850 Bab alirudishwa Tabriz akawekwa mbele ya kikosi cha wanajeshi ambao walimpiga risasi. Maiti yake ilitupwa katika shimo. Maiti yake ilichukuliwa kwa siri usiku na wafuasi wake na kufichwa baadaye katika sehemu mbalimbali hadi alipoletwa Haifa mnamo 1899 na alilazwa na ʿ Abdul-Baha ' katika jengo la kaburi kwenye Mlima Karmeli mnamo 1909. ![]() Wafuasi wakeBaada ya kifodini chake jumuiya aliyoanzisha iliendelea. Wafuasi wengi walijiunga na Baha 'u' llah aliyejitangaza kuwa yule aliyetangazwa na Bab na kuanzisha dini ya Baha'i. Wengine walikaa peke yao na ibada za pekee lakini si wengi. Leo hii wako mnamo wafuasi 1,000 wanaoendelea katika mafundisho wa Bab ilhali hawakujiunga na Ubahai. Upeo wa kufichuaBab ameandika mengi. Yeye mwenyewe alisema mnamo 1848 kwamba alikuwa ameandika vifungu 500,000. Katika jamii ya Bahai kuna mkusanyo wa dondoo kutoka maandishi ya Bab katika lugha za Ulaya chini ya kichwa "Uteuzi kutoka kwa maandishi yake". Louis Alphonse Daniel Nicolas Karne ya alama saba na Bayan ya Kiarabu na Kiajemi iliyotafsiriwa kwa Kifaransa. Kazi zake muhimu zaidi ni:
Ushuhuda wa mtu binafsi
Kutoka kwa Bab
Juu ya Bab
Viungo vya nje
|