Zimbabwe
JinaJina Zimbabwe linatokana na neno "dzimba dzamabwe" linalomaanisha "nyumba ya mawe" kwa lugha ya Kishona. Nyumba hiyo ya mawe, ambayo imehifadhiwa kama eneo la kihistoria, ilikuwa makao ya Ufalme wa Mutapa ambaye mfalme wake aliongoza eneo hilo miaka ya kale. ![]() ![]() EneoZimbabwe imegawiwa katika mikoa 8 na miji 2 yenye hadhi ya mikoa. Imegawiwa zaidi katika wilaya 64 na kata 1,970.
Miji minne mikubwa ya Zimbabwe ni:
![]() ![]() HistoriaHistoria ya awaliWakazi wa kwanza huaminiwa kuwa wawindaji wa jamii ya Wasani. Katika karne za kwanza BK walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi. Tangu karne ya 11, Zimbabwe ya leo imekuwa na falme imara kwenye njia muhimu ya biashara, hasa ufalme wa Mutapa. UkoloniKampuni ya British South Africa ya Cecil Rhodes iliweka mipaka ya sasa katika miaka ya 1890. Koloni la Uingereza lilianzishwa mwaka 1923 kwa jina la Southern Rhodesia. Mwaka 1965, serikali ya walowezi Wazungu ilijitangazia uhuru kwa jina la Rhodesia tu. Baada ya miaka 14 ya kutengwa kimataifa na kupigana na raia Waafrika katika miaka ya 1970, mapatano ya mwaka 1979 yalikubali wakazi wote wawe na haki ya kupiga kura na nchi ikawa huru kweli kwa jina la Zimbabwe mwaka 1980. Baada ya uhuruRais Robert Mugabe alipata umaarufu katika siasa kama mpiganaji dhidi ya ukoloni lakini pia kama aina ya dikteta aliyerudisha nyuma uchumi wa nchi. Baada ya yeye kulazimishwa na wanajeshi kujiuzulu, tarehe 24 Novemba 2017 Emmerson Mnangagwa amekuwa rais mpya wa Zimbabwe. DemografiaKabilaWakazi wengi (82%) ni wa kabila la Washona, 14% ni Wandebele, 3% ni wa makabila mengine ya Kiafrika, 0.2% ni Wazungu, 0.1% ni machotara, n.k. LughaKwa sasa lugha rasmi ni 16. Lugha kubwa ni Kishona (70%) na Kindebele (20%). Kiingereza ni lugha ya kwanza ya chini ya asilimia 2.5% za wakazi. DiniUpande wa dini, 84.1% ni Wakristo (hasa Waanglikana, Wakatoliki 8%, Wasabato na Wamethodisti). Waliobaki ni wafuasi wa dini asilia za Kiafrika (4.5%), ni Waislamu (0.7%), au hawana dini (10.2%) . Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya njeSerikali
Habari
WanamgamboMaelekezo
Utalii
Nyingine
|