Guinea
Imepakana na Gine-Bisau, Senegal na Mali upande wa kaskazini, Kodivaa, Liberia na Sierra Leone kusini halafu Bahari ya Atlantiki upande wa magharibi. Eneo lake ni chanzo ya mito mikubwa ya Niger, Senegal na Gambia. JinaJina la "Gine" liliwahi kutaja sehemu kubwa ya Afrika ya Magharibi kati ya jangwa la Sahara na Ghuba ya Gine ya Atlantiki likimaanisha "nchi ya watu weusi" kwa lugha ya Kiberberi. WatuMakabila yaliyopo nchini ni 24. Kubwa zaidi ni lile la Wafulani (40%). Lugha rasmi ni Kifaransa, lakini wakazi wanatumia zaidi lugha asilia kadiri ya makabila, hasa Kipular, Kimandinka, Kisusu, Kikisi, Kikpelle na Kiloma, Upande wa dini, 85% ni Waislamu (hasa Wasuni), 8% ni Wakristo (hasa Wakatoliki) na 7% ni wafuasi wa dini asilia za Kiafrika. Picha
Tazama pia
Viungo vya njeSerikali
Habari
Muziki
Orodha
|