Share to: share facebook share twitter share wa share telegram print page

Timbuktu

Msikiti ya kihistoria wa Djingerber
Geti la kale la Chuo Kikuu cha Sankore

Timbuktu (kwa Kifaransa: Tombouctou; kwa Kiarabu: تمبكتو) ni mji nchini Mali kusini mwa jangwa la Sahara kwa umbali wa takriban km 13 kutoka mto Niger. Leo kuna takriban wakazi 32,460 (2018).

Kituo cha biashara ya ng'ambo ya Sahara

Timbuktu imejulikana zaidi kutokana na historia yake. Katika enzi ya kati mji ulikuwa kituo muhimu cha biashara ya misafara kupitia Sahara na pia kuvuka kanda la Sahel kusini ya jangwa hadi Sudan na Misri. Wakati ule mji uliunganishwa na mto Niger kwa mfereji ulioruhusu mashua ya biashara kufika sokoni moja kwa moja kwa njia ya maji. Wakati ule mji ulikuwa na wakazi 100,000.

Utaalamu wa Kiislamu

Utajiri wa mji ulisaidia kujenga utamaduni wa kitaalamu. Kuna habari za madrasa 180 wakati moja. Hadi leo chuo kikuu cha Sankore ni dalili ya urithi huo kinaendelea kufanya kazi.

Baada ya kutekwa na Wamoroko mnamo 1591 Timbuktu haukustawi tena. Sababu muhimu pamoja na vita ni pia mabadiliko ya biashara; jahazi kwenye Atlantiki zilichukua sehemu kubwa ya biashara ya misafara kuvuka jangwani.

Timbuktu ilitembelewa mnamo mwaka 1510 na msafiri Mwarabu aliyejulikana baadaye kwa jina la Leo Africanus aliyepeleka habari za Timbuktu hadi Ulaya.

Timbuktu iliingizwa katika orodha ya urithi wa dunia ya UNESCO tangu 1988.

Leo hii ni mji maskini unaotembelewa na watalii wachache wanaotafuta dalili za enzi za kale.

Tazama pia

Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Timbuktu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Kembali kehalaman sebelumnya