Pythagoras![]() ![]() Pythagoras (kwa Kigiriki Πυθαγόρας; mnamo 570 KK - baada ya mwaka 510 KK) alikuwa mtaalamu wa falsafa na hisabati wakati wa ustaarabu wa Ugiriki ya Kale. MaishaAlizaliwa kisiwani Samos karibu na pwani ya Asia Ndogo. Alipokuwa na umri wa miaka 14 alihamia Italia ya kusini iliyokuwa eneo lenye miji mingi ya Wagiriki wa Kale. Pythagoras anakumbukwa hasa kwa "uhakiki wa Pythagoras" unaoeleza tabia za pembetatu mraba. Aligundua ya kwamba mraba juu ya hipotenusi (kiegana au upande kinyume cha pembe mraba) ni sawa na jumla ya miraba juu ya pande mbili nyingine. Pythagorasi alianzisha kundi la kidini la wanahisabati; walitafuta siri za dunia katika namba wakiamini ya kwamba miungu walificha habari za dunia ndani ya namba zinazoonekana kote duniani kwa wataalamu wa hisabati hii takatifu. Wanafunzi wake walifundisha uhamisho wa roho za watu kutoka mwili mmoja kwenda mwili mwingine; miili hufa, lakini roho zadumu. Pythagorasi alidai ya kwamba yeye alikumbuka maisha yake manne ya awali. Alikataa kuua wanyama kwa sababu aliona roho ndani ya wanyama pia, hivyo wanafunzi wake hawakula nyama.
|