Mawimbi ya nuru huwa na masafa ya nanomita 380 hadi 780 au yenye marudio ya takriban terahezi 789 hadi 384.
Chanzo cha nuru duniani ni hasa jua. Nuru ya jua inaleta pia nishati inayotumiwa na mimea ambayo kwa njia ya usanisinuru inajenga kwa ndani sukari au wanga ambavyo ni lishe za viumbehai vyote vinavyozila. Hivyo nuru ya jua, kwa njia ya usanisinuru, ni chanzo cha nishati kwa karibu viumbehai vyote duniani.
Chanzo kingine cha nuru kwa binadamu ni moto. Lakini hadi karne ya 19 nuru hii ilitumia pia nishati ya jua iliyotunzwa na mimea kwa njia ya kuni, mafuta ya petroliamu au gesi asilia. Ni tangu kugunduliwa kwa umeme tu ya kwamba chanzo tofauti cha nuru kimepatikana.
Nuru kama mnururisho
Nuru inayoonekana kwetu ni sehemu ya mnururisho wa sumakuumeme. Nuru inayoonekana ni sehemu ndogo tu ya spektra ya sumakuumeme.
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nuru kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.