Lishe huhusisha kuliwa kwa chakula, madini na virutubishi kuchukuliwa mwilini, madini na virutubishi kutumiwa na seli za mwili, hali kadhalika kuondolewa kwa uchafu katika mwili.
Lishe ni chakula ambacho mnyama yeyote hula huambatana na jinsi kinavyopatikana. Katika binadamu lishe huhushisha maandalizi ya chakula, jinsi ya kukihifadhi na jinsi ya kuzuia chakula kupata hali mbovu ambayo yanaweza kuleta maradhi kwa binadamu.
Magonjwa yanayotokana na lishe hafifu
Katika binadamu chakula chenye upungufu wa virutubishi na madini chaweza kusababisha maradhi kama vile upungufu wa damu mwilini, upofu, kutoka damu kwa fizi, kuzaliwa kwa mtoto kabla ya wakati kuwadia na mtoto kuzaliwa kama amekufa.
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Lishe kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.