Share to: share facebook share twitter share wa share telegram print page

Maktaba

Maktaba ya Abasia ya Melk nchini Austria.
Halifax Central Library, mfano wa maktaba ya kisasa.
Ukumbi wa kujisomea katika maktaba ya New York City.

Maktaba ni sehemu au jengo lililo maalum kwa ajili ya kujisomea na kujifunza juu ya vitu mbalimbali. Kuna aina kadhaa za maktaba ila zote hazina tofauti kwani zina lengo moja: kutoa elimu.

Asilimia kubwa ya maktaba huwa na vitabu vya aina mbalimbali, kwa mfano: vya kiada na ziada.

Pia unaweza kuwa na maktaba yako binafsi na licha ya kuwa na maktaba yako unaweza kwenda shuleni ukaingia maktaba kwani kuna maktaba ya shule.

Pia kuna maktaba ya kijiji, ya wilaya, ya mkoa na hata ya taifa, zote hizi kwa ajili ya elimu.

Historia

Historia ya maktaba ilianza na jitihada za kupanga na kuhifadhi hati. Maktaba za mwanzo kabisa zilikuwa hifadhi za maandiko ya kale yaliyoandikwa kwa mwandiko wa kikabari kwenye vigae huko Sumer, ambavyo vingine vinarudi hadi mwaka 2600 KK.

Maktaba za binafsi zilizo na vitabu zilianza kuonekana Ugiriki ya Kale karne ya 5 KK.[1]

Ilipofikia karne ya 6 BK, mwishoni mwa kipindi cha Kale, maktaba maarufu zaidi katika dunia zilikuwa zile za Konstantinopoli na Aleksandria. Pia, dola la Wafatima (9091171) lilikuwa na maktaba kubwa na mashuhuri, kama ile ya ikulu ambayo Ibn Abi Tayyi’ aliielezea kuwa ajabu la dunia.

Katika historia, pamoja na mauaji ya kikatili, uharibifu wa maktaba umekuwa silaha ya makusudi kwa washindi waliotaka kufuta kumbukumbu za jamii zilizoshindwa. Mfano mashuhuri ni mauaji ya Wamongolia dhidi ya Nizaris huko Alamut mwaka 1256 na kuchomwa kwa maktaba yao mashuhuri, ambayo umaarufu wake ulienea kote duniani, kwa mujibu wa Juwayni, mmoja wa washindi.

Maktaba za Timbuktu zilianzishwa karne ya 14 na zilivutia wasomi kutoka sehemu mbalimbali za dunia.[2]

Maktaba ya kisasa ya kwanza ya umma ilikuwa Maktaba ya Załuski (Biblioteka Załuskich), iliyoanzishwa mwaka 1732 huko Warshawa, Polandi-Lithuania, na baadaye ikawa Maktaba ya Kitaifa ya Polandi.[3]

Tanbihi

  1. Pfeifer, Wolfgang (1989). Etymologisches Wörterbuch des Deutschen. A-G. Berlin: Akademie-Verlag. uk. 166. ISBN 3-05-000641-2.
  2. Virani, Shafique N. (2007-04-01). The Ismailis in the Middle Ages. Oxford University Press. doi:10.1093/acprof:oso/9780195311730.001.0001. ISBN 978-0-19-531173-0. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Novemba 2021. Iliwekwa mnamo 22 Juni 2021.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Singleton, Brent D. (2004). "African Bibliophiles: Books and Libraries in Medieval Timbuktu". Libraries & Culture. 39 (1): 1–12. doi:10.1353/lac.2004.0019. ISSN 1932-4855. JSTOR 25549150. S2CID 161645561. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 19 Agosti 2020. Iliwekwa mnamo 2022-01-19.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Kembali kehalaman sebelumnya