Kimelea![]() Kimelea (pia: kidusia[1]; kwa Kiingereza parasite) ni kiumbehai ambaye anaishi ndani au juu ya kiumbehai mwingine wa spishi tofauti na kupata virutubishi kutokana na mwili wa kiumbe huyo, ambaye kwa kawaida ni mkubwa zaidi, bila kumpa kiumbe mwenyeji faida yoyote. Kinyume chake, mara nyingi analeta hasara au kusababisha ugonjwa. Vimelea vingi ni vidogo sana vikiishi ndani ya wanyama au binadamu. Aina za vimeleaVimelea vingine ni vikubwa kiasi cha kuonekana kwa jicho:
Vimelea vingine ni vidogo mno, vinaonekana kwa hadubini tu:
Vimelea kati ya mimea na wanyamaKuna pia wanyama wakubwa zaidi wanaotumia mbinu za kimelea kwa mfano ndege kama vile kekeo, fumbwe au kinili wanaotega mayai katika matego ya spishi nyingine. Kuna mimea inayopata lishe kwa kutumia moja kwa moja majimaji ya mimea mingine na aina kadhaa kati ya hizi zinaendelea bila kutumia usanisinuru kabisa. Vimelea na wenyeji waoVimelea mara nyingi hudhoofisha viumbehai wenyeji wao vinamoishi na vinaweza kusababisha magonjwa; kwa kawaida haviwaui mara moja, maana kimelea kinachomwua mwenyeji wake kitakosa mahali pa kuishi. Vimelea vingi vinahitaji mazingira ya mwili wa spishi fulani vikiweza kuishi hapo tu. Vimelea nje ya mwili wa mwenyejiVimelea hawa ni kama chawa, kunguni na kupe ambao huishi nje ya mwili wa mwenyeji (ecto-parasites) na hufyonya damu na kutaga mayai juu yake. Huenda wakasambaa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Wao hungojea mwenyeji aje karibu nao ambapo wanamnata na kuanza kumtegemea kwa lishe na pia kwa pahala pa kuzalisha. Marejeo
Kujisomea
Viungo vya nje
|