Kaunti ya Kitui
Kwa makao makuu, soma Kitui
Kaunti ya Kitui ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010 .
Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 1,136,187 katika eneo la km2 30,429.5, msongamano ukiwa hivyo wa watu 37 kwa kilometa mraba [ 1] .
Makao makuu yako Kitui .
Jiografia
Kaunti ya Kitui inapakana na kaunti za Tana River , Taita Taveta , Makueni , Machakos , Embu na Tharaka Nithi . Ina hali ya tabianchi kavu na nusu kavu . Ina vilima na ardhi tambarare. Kitui hupata misimu miwili ya mvua, Machi hadi Mei na Oktoba hadi Disemba.
Utawala
Kitui imegawanywa katika maeneo bunge yafuatayo[ 2] :
Eneo bunge
Kata
Mwingi Kaskazini
Ngomeni , Kyuso , Mumoni , Tseikuru , Tharaka
Mwingi Magharibi
Kyome/Thaana , Nguutani , Migwani , Kiomo/Kyethani
Mwingi ya Kati
Mwingi ya Kati , Kivou , Nguni , Nuu , Mui , Waita
Kitui Magharibi
Mutonguni , Kauwi , Matinyani , Kwa Mutonga/Kithumula
Kitui Rural
Kisasi , Mbitini , Kwa Vonza/Yatta , Kanyangi
Kitui ya Kati
Miambani , Kitui Mjini , Kyangwithya Magharibi , Mulan , Kyangwithya Mashariki
Kitui Mashariki
Zombe/Mwitika , Nzambani , Chuluni , Voo/Kyamatu , Endau/Malalani , Mutito/Kaliku
Kitui Kusini
Ikanga/Kyatune , Mutomo , Mutha , Ikutha , Kanziko , Athi
Idadi ya wakazi katika kaunti ndogo (2019) [ 3]
Ikutha 82,964
Katulani 47,108
Kisasi 46,142
Kitui Central 105,991
Kitui West 70,871
Kyuso 76,867
Lower Yatta 63,329
Matinyani 47,811
Migwani 79,255
Mumoni 29,344
Mutitu 55,287
Mutitu North 21,215
Mutomo 113,356
Mwingi Central 108,713
Mwingi East 85,139
Nzambani 46,788
Thagicu 15,136
Tseikuru 40,871
Tazama pia
Marejeo
↑ "Nakala iliyohifadhiwa" . Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30 .
↑ "Kitui County Assembly - Wards" . Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-04-12. Iliwekwa mnamo 2018-04-17 .
↑ "Nakala iliyohifadhiwa" . Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30 .
Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kaunti ya Kitui kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari .