Chandra Shekhar Azad![]() Chandra Shekhar Azad (linatamkwa pia Chandrasekhar; anajulikana kwa wengi kwa jina la Azad, yaani "Uhuru"; 23 Julai 1906 – 27 Februari 1931), ni mwanamapinduzi wa India aliyekipanga tena chama cha The Hindustan Republican Association chini ya jina jipya la Hindustan Socialist Republican Association (HSRA) baada ya kifo cha mwanzilishi wake, Ram Prasad Bismil, na viongozi wengine watatu, Roshan Singh, Rajendra Nath Lahiri na Ashfaqulla Khan. Mara nyingi alikuwa akitia saini nyaraka za jeshi la HSRA kwa jina la "Balraj" .[1] Maisha ya awaliAzad alizaliwa kama Chandrashekhar mnamo 23 Julai 1906 katika kijiji cha Bhabhra. Babu zake walitokea katika kijiji cha Badarka karibu na Kanpur, na mama yake Jagrani Devi Tiwari, alikuwa mke wa tatu wa Sitaram Tiwari, ila wake zake wa kwanza walikufa katika umri wa ujana. Baada ya kuzaliwa kwa mtoto wake wa kwanza, Sukhdev, huko Badarka, familia ya Sitaram iliamua kuhamia Alirajpur.[2][3] Mama yake alitaka mtoto wake awe msomi mkubwa wa Sanskrit akamshawishi baba yake ampeleke kwa Kashi Vidyapeeth, Banaras, kusoma, mnamo Disemba 1921, wakati huo Mohandas Karamchand Gandhi alikuwa akizindua Non-Cooperation Movement, Chandra Shekhar, alijiunga. Akiwa na umri wa miaka 15 alikamatwa na kupelekwa mahakamani na baada yA hapo ndipo alikuja kufahamika kwa jina jipya la Azad lenye kumaanisha uhuru katika lugha ya Kihindi.[4] Maisha ya KimapinduziBaada ya kusimamishwa kwa harakati za non-cooperation movement (harakati za kutoshirikiana na Waingereza), mwaka 1922, Azad alikutana na mwanamapinduzi kijana, Manmath Nath Gupta, ambaye ndiye aliyemtambulisha kwa Ram Prasad Bismil ambaye alikuja kuanzisha The Hindustan Republican Association (HRA), na kuwa mwanachama hai ambaye alishiriki kwa asilimia kubwa kukusanya pesa za HRA ambazo walizipata kwa njia ya wizi wakiibia serikali. Anahusishwa pia na wizi katika treni ya Kakori mwaka 1925. Watu wengine kama Motilal Nehru mara kadhaa walikuwa wakitoa pesa ili kumuunga Azad mkono katika harakati zao.[5] Marejeo
|