Walter CiszekWalter Joseph Ciszek, S.J., (4 Novemba 1904 – 8 Desemba 1984) alikuwa mtawa wa shirika la Wajesuiti na padri wa Kanisa Katoliki la Kigiriki la Russia mwenye asili ya Polandi kutoka Marekani ambaye alifanya kazi ya kichungaji kwa siri katika Umoja wa Kisovyeti kati ya miaka 1939 na 1963. Miaka kumi na tano kati ya hiyo aliishi kwa kifungo na kazi ngumu katika Gulag, pamoja na miaka mitano iliyotangulia hiyo katika gereza maarufu la Lubyanka huko Moscow. Aliachiliwa na kurudi Marekani mwaka 1963, ambapo aliandika vitabu viwili, He Leadeth Me na kumbukumbu With God in Russia, na alihudumu kama kiongozi wa kiroho.[1] Tangu mwaka 1990, maisha ya Ciszek yamekuwa chini ya tathmini na Kanisa Katoliki kwa ajili ya kumtangaza mtakatifu. Hadi mwaka 2024, anaitwa Mtumishi wa Mungu. Marejeo
|