Ua
![]() Maua ni majani ya pekee kwenye sehemu za uzazi wa mimea. Mara nyingi kwa nje huwa na rangi za kuvutia na kwa sababu hii maua yanapendwa pia na wanadamu kama mapambo. Katika lugha ya kila siku neno "ua/maua" linataja pia mmea wote wenye maua. PetaliMajani ya nje au petali yanayoonekana vizuri pamoja na rangi yake huitwa petali. Huwa na rangi mbalimbali ili kuvuta wadudu wanaochavusha ua na hivyo kuusaidia mmea kuzaa. Yanaviringisha na kukinga viungo vya uzazi ndani yake. ![]() 1 kombe, 2 Sepali, 3 Petali, 4 Stameni zenye chavulio na filamenti, 5 Pistili yenye stigma, staili na ovari Viungo vya uzaziViungo hivi kimsingi ni vya aina mbili: ![]() StameniStameni huwa na pande mbili: PistiliPistili au sehemu ya kike huwa na sehemu tatu: ![]() Pistili zimeundwa kwa kapeli moja au kadhaa ambazo ni aina za majani maalumu yanayobeba ovari. Ovari na mbeguBaada ya utungishaji ua hukauka na mbegu inakua ndani ya ovari. Kwa mimea kadhaa ovari inaendelea kuwa tunda linalotunza mbegu ndani yake; kusudi la tunda ni kuvuta wanyama wanaokula tunda na kusambaza mbegu kwa njia hii. JinsiaMimea mingi huunganisha sehemu za kike na za kiume ndani ya ua moja; mfano ni ua la waridi. Kuna pia mimea yenye maua ambayo ni ama ya kike au ya kiume, kwa mfano maua ya mtango au mboga. Viungo vya nje
|