Stratolaunch Roc![]() Stratolaunch Roc (ing. en:Scaled Composites Stratolaunch "Roc") ni eropleni kubwa zaidi duniani tangu kuruka mara ya kwanza katika mwezi wa Aprili 2019[1]. MfumoNdege hii imetengenezwa kwa kutumia ndege mbili za Boeing 747-400 ilhali injini, chumba cha rubani, magurudumu na haidroli za ndege hizi ilitumiwa. Ndege mpya ina upana mkubwa wa mabawa wa mita 117. Chini ya mabawa kuna sehemu mbili za pekee, na mzigo wa roketi utabebwa katikati chini ya mabawa[2]. Marubani hutumia chumba kwenye sehemu ya kulia, ilhali chumba cha rubani upande mwingine ni tupu. Hata kama Stratolaunch Roc ni ndege kubwa duniani kufuatana na vipimo vyake, ndege ya Antonov An-225 kutoka Ukraine inabeba mzigo ulio sawa[3][4]. Kurusha hewaniIlijengwa na kampuni ya Stratolaunch Systems kwa kusudi la kubeba roketi zinazorushwa hewani na kulenga anga-nje. Mbinu huu unapunguza gharama kwa kurusha roketi kuanzia kimo cha mita 10,500.[5] JinaIlhali stratolaunch ni jina la kampuni, Roc ni kifupi cha "rocket carrier" na wakati huohuo mchezo wa neno maana katika fasihi ya Uarabuni na Ulaya ndege-dubwana Rok (pia Roc, Rokh au Rukh, ar. رُخّ rukh) alikuwa ndege mkubwa wa ajabu anbaye chakula chake kilikuwa tembo, pia aliweza kubeba jahazi pamoja na watu wake. Marejeo
Viungo vya Nje
|