SentensiSentensi ni kundi la maneno ambalo lina kiima na kiarifa na hutoa maana kamili; ndiyo kipashio cha juu kabisa katika tungo. Aina za sentensiKuna aina kuu nne za sentensi nazo ni:
1. Sentensi sahili - Hii ni aina ya sentensi iliyoundwa kwa kishazi huru kimoja tu, mfanoː Mama anakula. 2. Sentensi changamano - Hii ni aina ya sentensi iliyoundwa kwa kishazi tegemezi na kishazi huru, mfanoː Mtoto aliyepotea ameonekana. 3.Sentensi ambatano - Hii ni aina ya sentensi iliyoundwa kwa sentensi mbili zilizounganishwa na kiunganishi, mfanoː Baba analima ingawa mama anakula. Sentensi ambatano huweza kuundwa kwaː a. sentensi sahili + sentensi sahili. b. Sentensi sahili + sentensi changamano. c. Sentensi changamano + sentensi changamano. 4. Sentensi shurutia - Hii ni aina ya sentensi iliyoundwa kwa mofimu za masharti, mfanoː ki, nge, ngeli pamoja na ngali. Njia za uchanganuzi wa sentensiː a. Njia ya matawi au ngowe. b. Njia ya mishale au mistari. c. Njia ya visanduku au jedwali. d. Njia ya maneno. Hatua za uchanganuzi wa sentensiː 1. Kuainisha sentensi husika 2. Kugawa sentensi katika kiima na kiarifu 3. Kuonesha vipashio vya kiima na kiarifu 4. Kuainisha aina za maneno 5. Kuandika sentnsi husika kwa kila panapohusika Muundo wa sentensiSentensi huundwa kwa sehemu kuu mbili: Tazama pia
|