Rula
![]() Rula (kutoka Kiingereza ruler) ni kifaa kinachotumika kupima urefu. Kizio cha kawaida cha kupima urefu ni Mita (m). Hata hivyo, mita si kizio pekee cha kupima urefu, kuna vizio vingine kama vile Kilometa, sentimeta, Milimita na vilevile Maili n.k. ambayo hutumika kupika urefu. AinaRula hutengenezwa kwa aina mbalimbali na urefu tofauti. Baadhi ni za mbao, chuma au plastiki. Rula fupi ni bora kwa kuweka mfukoni, wakati nyingine ni ndefu kwa matumizi mbalimbali. Historia![]() Rula zilianza kutumika miaka mingi iliyopita. Ufito wa shaba wa kupimia wa kale kabisa ni wa mwaka 2650 KK na ulivumbuliwa na Mjerumani Eckhard Unger huko Nippur. Rula zilizotengenezwa kwa pembe ya ndovu zilitumiwa kwenye Ustaarabu wa Bonde la Indus kabla ya 1500 KK. Rula ya aina hii ilipatikana wakati wa uchimbaji huko Lothal (2400 KK) ikiwa na milimita 1.6. Anton Ullrich alivumbua rula ya kukunja mwaka 1851. Frank Hunt alivumbua rula inayopindika mwaka 1902.[1] Faida za rula1) hutumika kupima urefu wa kitu 2) hutumika katika kuchora Marejeo
|