Queen Nwokoye![]() Queen Nwokoye (amezaliwa 11 Agosti 1982) ni mwigizaji wa Nigeria.[1][2] Anajulikana sana kwa kuigiza kama mhusika katika filamu inayoitwa "Chetanna" mwaka 2014 ambayo ilimpatia uteuzi wa" Mwigizaji Bora "katika Tuzo za 11 za Filamu za Afrika.[3] Maisha ya mwanzo na elimuNwokoye alizaliwa katika jimbo la Lagos katika familia ya Kikatoliki lakini anatoka Ihembosi katika serikali ya mtaa ya Ekwusigo ya jimbo la Anambra Nigeria).[4] Alianza Elimu yake katika shule ya msingi ya Air Force. Alimaliza masomo yake ya sekondari katika chuo cha Queen, Enugu kabla ya kwenda chuo kikuu cha Nnamdi Azikiwe Awka, Anambra State ambapo alisoma sosholojia na anthropolojia. Alitamani ya kuwa wakili.[4] KaziTangu aanze kuigiza mnamo 2004 katika filamu inayoitwa "Nna Men", Nwokoye ameendelea kuigiza katika filamu kadhaa za Nigeria, akishinda tuzo na kupata jina.[5][6] Maisha binafsiQueen Nwokoye ameolewa na Bwana Uzoma na wamejaliwa watoto watatu wavulana mapacha[7] na binti mmoja. Marejeo
|