Teolojia katika dini mbalimbali inatumia neno hili kadiri ya imani yake maalumu.
Kwa namna ya pekee neno linatiwa mkazo katika Ukristo unaosisitiza kwamba mambo yote ni neema (kwa Kigiriki: χάρις, kharis; kwa Kilatini: gratia, yaani deso, kitu cha bure).
Hata hivyo madhehebu yake yanatofautiana sana katika kutafsiri tamko hilo.
Katika Kanisa Katoliki
Neema ni msaada wowote tunaopewa bure na Mungu ili tupate kufika mbinguni. (Lk 1:30; Rum 5:2,20; Fil 2:13)
Vilevile linasadiki kwamba Roho Mtakatifu ndiye anayetugawia neema hizo kwa ajili ya Kanisa. (Yoh 1:16; 3:3-8) na kwamba mtu anaweza kujipatia neema kwa njia ya sakramenti, sala na matendo mema. (Yak 5:16-20)
Neema ni za aina mbalimbali:
neema za sakramenti
neema za pekee kama vile karama na zile zinazotusaidia kutimiza majukumu yetu maalumu
Neema za msaada ni fadhili mbalimbali ambazo Roho Mtakatifu anasaidia akili na utashi wa mtu kuanza, kuendeleza na kutimiza kazi ya wokovu wake kwa kutenda mema na kuepuka mabaya. (Yoh 15:5; Fil 2:13; 1Tim 2:4)
Neema ya utakaso ndiyo muhimu zaidi kwa sababu ni uzima wa Mungu unaotiwa rohoni mwa mtu aweze kutenda kwa upendo wake na kujiandaa kuishi naye milele. (Yoh 1:16; 3:3-8; Ef 3:4-7; 2Pet 1:3-4)
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.