Share to: share facebook share twitter share wa share telegram print page

Martha Kim Songim

Martha Kim Songim (Pupyeong, 1787 - Seoul, 20 Julai 1839) alikuwa Mkristo wa Rasi ya Korea aliyeuawa pamoja na Magdalena Yi Yonghui, Teresa Yi Maeim, Lusia Kim Nusia, Rosa Kim Nosa, Ana Kim Changgum, Maria Won Kwiim, na Yohane Mbatizaji Yi Kwangnyol [1].

Ni mmojawapo katika kundi kubwa la Wakristo wa Kanisa Katoliki nchini Korea waliouawa kwa ajili ya imani yao katika miaka 17911888. Wanakadiriwa kuwa 8,000 - 10,000.

Yeye[2] na wenzake 102 walitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa watakatifu tarehe 6 Mei 1984.[3]

Sikukuu ya hao Wafiadini wa Korea pamoja huadhimishwa tarehe 20 Septemba, lakini ya kwake mwenyewe tarehe ya kifodini chake [4].

Mazingira

Mwishoni mwa karne ya 18, Ukristo wa Kikatoliki ulianza kuenea taratibu nchini[5] kwa juhudi za wananchi walei. Mwaka 1836 Korea, nchi ya Kikonfusyo ilipata wamisionari wa kwanza kutoka nje (wanashirika wa Paris Foreign Missions Society)[6].

Chini ya nasaba ya Joseon, Ukristo ulifutwa, tena waamini walidhulumiwa na kuuawa. Waliobaki walipaswa kushika imani yao kwa siri.

Tazama pia

Tanbihi

  1. https://www.santiebeati.it/dettaglio/63720
  2. https://www.santiebeati.it/dettaglio/63720
  3. "Korea and the church of martyrs". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-01-25. Iliwekwa mnamo 2020-04-06.
  4. Martyrologium Romanum
  5. Michael Walsh, ed. "Butler's Lives of the Saints" (HarperCollins Publishers: New York, 1991), p. 297.
  6. The Liturgy of the Hours Supplement (New York: Catholic Book Publishing Co., 1992, pp. 17–18.

Marejeo ya Kiswahili

  • John Kabeya na wengine - Maisha ya Watakatifu – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1965, 1989, uk. 327-329
  • Pd. Leandry Kimario, O.F.M.Cap. - Mfahamu Mtakatifu Somo Wako - Maisha ya Watakatifu wa Kila Siku pamoja na Watakatifu Wafransisko - Toleo la pili - Dar es Salaam 2021, uk. 282-283

Marejeo ya lugha nyingine

Viungo vya nje

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
Kembali kehalaman sebelumnya