Luanda
![]() ![]() ![]() Luanda (kirefu: São Paulo de Luanda: pia Loanda) ni mji mkuu pia mji mkubwa wa Angola ikiwa na wakazi 2,487,484 (katika rundu la jiji 7,805,000) wanaongezeka haraka kutoka ndani na nje ya nchi na ya bara la Afrika. JiografiaMji wa Luanda uko mkoani Luanda, kaskazini ya mdomo wa mto Cuanza mwambaoni pa Atlantiki. HistoriaMji ulianzishwa na Wareno mwaka 1575 BK kwa jina la São Paulo de Luanda. Umekuwa mji mkuu wa Angola tangu mwaka 1627. Hadi mwaka 1850 Luanda ilikuwa kitovu cha biashara ya watumwa kwenda Brazil. Wakati wa uhuru mwaka 1975 walowezi wengi Wareno waliondoka mjini. Vita ya wenyewe kwa wenyewe katika Angola kati ya miaka 1974 - 2002 ilileta hasara pia kwa mji mkuu. WakaziKati ya wakazi, walio wengi kabisa ni Waafrika wa makabila kama vile Waovimbundu, Wakimbundu na Wakongo. Lugha rasmi ni Kireno lakini lugha nyingi za Kibantu zinatumika pia. UchumiLuanda ni bandari muhimu nchini pia mwanzo wa reli kwenda Malange. Viungo vya nje
|