Louis Martin![]() ![]() Louis Martin (Bordeaux, Gironde, Ufaransa, 22 Agosti 1823 - Arnières-sur-Iton, Eure, Ufaransa, 29 Julai 1894) alikuwa mwanamume Mkristo wa Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko. Pamoja na mke wake, Marie-Azélie Guérin, alitangazwa na Papa Benedikto XVI kuwa mwenye heri tarehe 19 Oktoba 2008, halafu Papa Fransisko alimtangaza mtakatifu tarehe 18 Oktoba 2015. Ni maarufu hasa kutokana na mtoto wao wa tisa na wa mwisho, mtakatifu Teresa wa Mtoto Yesu, O.C.D., bikira na mwalimu wa Kanisa, aliyeandika vizuri ajabu juu ya uadilifu wao. MaandishiMwaka 2011 barua 216 za Zélie na 16 za Louis Martin zilitolewa kwa Kiingereza katika kitabu A Call to a Deeper Love: The Family Correspondence of the Parents of Saint Therese of the Child Jesus, 1863–1885 (ISBN 0818913215). Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
|