Kitabu cha Yoshua bin SiraKitabu cha Yoshua bin Sira ni kimojawapo kati ya vitabu vya deuterokanoni vya Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo. Mwandishi alikuwa Myahudi wa Yerusalemu aliyetunga kitabu chake kwa Kiebrania mnamo miaka 196 KK - 175 KK huko Aleksandria (Misri). Halafu mjukuu wake alikitafsiri kwa Kigiriki akitanguliza dibaji. Wakatoliki na Waorthodoksi wanakubali kama Neno la Mungu tafsiri hiyo, si maandiko asili. Ingawa kitabu hakionyeshi mara moja mpangilio mzuri, kwa kugusagusa mambo mbalimbali, mafundisho yake makuu ni kwamba Hekima, ambayo ni mamoja na Torati, ni sifa maalumu ya Wayahudi; hao tu wanaweza kumfikia Mungu. Kitabu kinatoa hasa maadili yanayofanana na yale ya Kitabu cha Mithali. Kama vitabu vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.
Vitabu vya Agano la Kale
Mwanzo * Kutoka * Walawi * Hesabu * Kumbukumbu * Yoshua * Waamuzi * Ruthu * Samueli I * Samueli II * Wafalme I * Wafalme II * Mambo ya Nyakati I * Mambo ya Nyakati II * Ezra * Nehemia * TobitiDK * YudithiDK * Esta * Wamakabayo IDK * Wamakabayo IIDK * Yobu * Zaburi * Methali * Mhubiri * Hekima DK * SiraDK * Wimbo Bora * Isaya * Yeremia * Maombolezo * BarukuDK * Ezekieli * Danieli * Hosea * Yoeli * Amosi * Obadia * Yona * Mika * Nahumu * Habakuki * Sefania * Hagai * Zekaria * Malaki Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.
|