Kikusa cha Uprogramishaji cha Programu tumiziKikusa cha Uprogramishaji cha Programu tumizi (kwa Kiingereza: Application Programming Interface, ufupi: API) ni kikusa kinachowezesha programu mbili tofauti kubadilishana data bila kujalisha tofauti katika utekelezaji wa michakato ya data katika hizo programu mbili. Mfumo ulio na API, hubainisha jinsi data itakavyopokelewa. Sehemu ya kupokea data huwa wazi na sehemu ya kuchakata data huwa dhahania, ikiwa imefichwa kwa watumizi wasio na ruhusa[1]. Seva ya API hufichua aina ya data, viumbile na kadhia zitakazopokelewa. Mteja hutuma data ikiwa katika fomati inayohitajika na seva. Kwa mfano, benki linaweza kuwa na API ambayo inaruhusu wateja kutuma ombi la salio. Katika kikusa, linaweza kuhitaji kuwepo kwa namba ya akaunti, msimbo wa usalama na jina la kadhia (ambalo ni ombi la salio). Seva itachakata kwa undani, kisha itoe jibu katika fomati iliyobainiwa. Ni wajibu wa mteja kujua fomati ili aweze kutuma data inavyofaa na programisha programu yake iweze kupokea majibu yatakayotolewa na seva. Marejeo
|