Kujifunza elimujamii ni kujifunza kuangalia dunia kwa mapana zaidi, yaani kutoka nje ya mipaka ya tafsiri zetu tulizojiwekea kijuujuu. Ni kukubali changamoto ya kuchunguza upya yale yote tunayoyajua kwa maana za kawaida: matokeo ya uchunguzi huo pengine hupingana na kile tulichokidhani mwanzoni na hivyo kutuwezesha kuuona ukweli katika hali mpya.
Elimujamii hutusaidia kuelewa hali halisi ya jamii ili kuchangia urekebishaji au utengenezaji wa sera mpya. Hutusaidia pia kukuza ujuzi wetu wa jamii mbalimbali na wa mahusiano yetu kijamii, yakiwa mazuri au mabaya vilevile. Hutusaidia tena kuelewa jumuia zetu kubwa au ndogo kama watu wanaoishi pamoja wakifuata mila na desturi za aina moja na kuwa na lengo moja. Hutusaidia kuelewa aina mbalimbali za utamaduni ili kurahisisha ushirikiano.
↑Des Manuscrits de Sieyès. 1773–1799, Volumes I and II, published by Christine Fauré, Jacques Guilhaumou, Jacques Vallier and Françoise Weil, Paris, Champion, 1999 and 2007. See also Christine Fauré and Jacques Guilhaumou, Sieyès et le non-dit de la sociologie: du mot à la chose, in Revue d'histoire des sciences humaines, Numéro 15, novembre 2006: Naissances de la science sociale. See also the article 'sociologie' in the French-language Wikipedia.
↑A Dictionary of Sociology, Article: Comte, Auguste
↑Macionis, Gerber, John, Linda (2010). Sociology 7th Canadian Ed. Toronto, Ontario: Pearson Canada. pp. 10.
Marejeo
Aby, Stephen H. Sociology: A Guide to Reference and Information Sources, 3rd edn. Littleton, Colorado, Libraries Unlimited Inc., 2005, ISBN 1-56308-947-5 OCLC 57475961
Coser, Lewis A., Masters of Sociological Thought : Ideas in Historical and Social Context, New York, Harcourt Brace Jovanovich, 1971. ISBN 0-15-555128-0.
Macionis, John J (1991). Sociology (tol. la 3rd). Englewood Cliffs, New Jersey: Prentice Hall. ISBN0-13-820358-X.
Merton, Robert K.. 1959. Social Theory and Social Structure. Toward the codification of theory and research, Glencoe: Ill. (Revised and enlarged edition) OCLC 4536864
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Elimujamii kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.