Chike AniakorChike C. Aniakor (alizaliwa tarehe 21 Agosti 1939) ni msanii, mwanahistoria wa sanaa, mwandishi, na mshairi wa Nigeria ambaye kazi yake inashughulikia mada za kifalsafa, kisiasa, na kidini zinazohusiana na jamii ya Igbo na watu wa Nigeria. [1] Maisha ya AwaliChike Cyril Aniakor alizaliwa Abatete, Jimbo la Anambra mashariki mwa Nigeria tarehe 21 Agosti 1939.[2] Mama yake alikuwa msanii wa Uli, mtindo wa sanaa unaotokana na utamaduni wa Igbo.[2] Ukaribu wake wa mapema na mila za Kiigbo ulimchochea kuvutiwa na ngoma zao, sanaa, desturi za ibada, pamoja na mitindo ya usanifu wa majengo ya jamii hiyo.[3] ElimuKuanzia mwaka 1960 hadi 1964, Aniakor alisoma katika Chuo cha Sanaa, Sayansi na Teknolojia cha Nigeria, Zaria, Jimbo la Kaduna (kilichokuja kubadilishwa jina kuwa Chuo Kikuu cha Ahmadu Bello, Zaria), ambako alipata shahada yake ya kwanza katika uchoraji.[2] Alifanya masomo yake ya uzamili katika Chuo Kikuu cha Indiana, Bloomington, ambako alipata shahada ya uzamili (1974) na shahada ya uzamivu (1978) katika historia ya sanaa.[4] Wakati akiwa Chuo Kikuu cha Indiana, michoro na mashairi yake yalionyeshwa katika maonyesho mengi ya sanaa, jambo lililompatia utambulisho wa umahiri na ufadhili wa kitaaluma, yakiwemo Tuzo la Rockefeller.[5] Baada ya kuhitimu, alifundisha katika Chuo Kikuu cha Kusini huko New Orleans, UCLA, na Chuo Kikuu cha Howard.[2] Tangu miaka ya 1970, amekuwa akifundisha sanaa na historia ya sanaa katika Chuo Kikuu cha Nigeria, Nsukka (UNN), Jimbo la Enugu, ambako alikua mwanachama mwanzilishi wa kikundi cha Nsukka, ambacho baadaye kilijulikana sana kwa matumizi ya mtindo wa sanaa wa Uli. Pia alikuwa mwanzilishi wa idara ya sanaa ya chuo kikuu hicho, ambayo ilisifiwa kwa umahiri wa wasomi na wanafunzi wake, pamoja na kuonyesha kazi za wasanii wao katika ulingo wa kimataifa wa sanaa.[6]
Marejeo
|