Cherero au kasuku-mapenzi ni ndege wa jenasi Agapornis katika familia Psittaculidae. Ndege hawa ni aina ya kasuku wadogo na wana rangi kali. Mkia wao ni mfupi kuliko kasuku wengine lakini kama hawa miguu yao ina vidole viwili vikabilivyo mbele na viwili vikabilivyo nyuma. Domo lao lina nguvu sana na mataya yamepindika kwa pande za kuelekea kama koleo. Cherero wanatokea Afrika na Madagaska. Hula matunda, mboga, mbegu na pengine wadudu. Dume na jike wanaishi pamoja kwa maisha yao yote. Hupitisha muda mrefu wakikaa karibu sana. Kwa hivyo huitwa kasuku-mapenzi pia. Jike huyataga mayai 3-8 tunduni kwa mti.
Spishi
Picha
-
Cherero kichwa-kijivu
-
Cherero kichwa-machungwa
-
Cherero wa Lilian
-
Cherero mashavu-meusi
-
Cherero shingo-njano
-
Cherero uso-mwekundu
-
Cherero uso-pinki
-
Cherero mkufu-mweusi
-
Cherero Habeshi
|
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Cherero kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
|