Kwa jumla hali ya hewa ni joto lenye unyevu. Handeni kuna joto kavu zaidi. Milima ya Usambara hakuna joto sana.
Miezi ya Desemba - Machihalijoto huko Tanga inafikia sentigredi 30-32 mchana na 26-29 usiku. Wakati wa Mei hadi Oktoba halijota inapoa: ni sentigredi 23-28 mchana na 20-24 usiku. Unyevu iko juu kati ya asilimia 100 na asilimia 65.
Maeneo mengi ya mkoa hupokea angalau milimita 750 za mvua kwa mwaka au zaidi. Pwani ni zaidi: takriban milimita 1,100 hadi 1,400 ikipungua sehemu za ndani isipokuwa milima ya Usambara ambako mvua inaweza kuzidi milimita 2000 kwa mwaka.
Wakazi
Mwaka 2022 wakazi waliohesabiwa katika sensa walikuwa 2,615,597 [1] kutoka 2,045,205 wa mwaka 2012[2].
Wazigua ni kabila kubwa huko Handeni na sehemu za Korogwe na Pangani. Wabondei wako hasa Muheza na sehemu za Pangani. Wadigo ndio wengi Tanga yenyewe na sehemu za pwani.
Elimu
Katika mkoa huu elimu inahitaji kuboreshwa zaidi, hasa maeneo ya vijijini, maana watu wengi wa mkoa huu hufanya shughuli zao za kimila na kushindwa kuendelea na zile za maendeleo katika taifa la Tanzania.
Katani ilikuwa zao la biashara hasa kwa ajili ya Tanga tangu kuingizwa kutoka Mexico zamani za Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Hulimwa kote mkoani isipokuwa Lushoto, hasa Muheza na Korogwe kwenye mashamba makubwa. Mashamba hayo yalikuwa ya walowezi, yakataifishwa baada ya uhuru. Tangu kuanguka kwa sekta ya umma yamebinafsishwa tena siku hizi. Zao la katani linategemea sana soko la dunia, umuhimu wake ulirudi nyuma tangu miaka ya 1960.
Tanga ilikuwa na viwanda vingi kiasi katika miaka ya 1960 na 1970 lakini karibu vyote vimekwama kutokana na siasa ya Ujamaa na uchumi wake ulioiga mfumo wa nchi za kisoshalisti. Viwanda vichache vilivyobaki havizalishi mali kulingana na uwezo wao. Kilichobaki hasa ni kiwanda cha saruji Tanga.
↑"Population Distribution by Administrative Units, United Republic of Tanzania, 2013"(PDF). National Bureau of Statistics, Ministry of Finance, Dar es Salaam and Office of Chief Government Statistician, President’s Office, Zanzibar. Machi 2013. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo(PDF) mnamo Juni 12, 2013. Iliwekwa mnamo 2017-08-22. {{cite web}}: More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tanga bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mkoa wa Tanga kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.