Stahili

Stahili (kutoka neno la Kiarabu) ni hali inayomfanya mtu awe na sifa ya kupata jambo fulani, jema au baya, hasa kutokana na matendo yake, kama ni mema au mabaya.

Katika dini mbalimbali, maadili yanafundisha namna ya kustahili tuzo kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Katika Ukristo kuna tofauti kubwa kati ya Wakatoliki na madhehebu mbalimbali ya Uprotestanti. Hata hivyo, baada ya mabishano ya muda mrefu, Wakatoliki na Walutheri wamefikia kuelewana[1] ; baadaye Wamethodisti pia wamesaini makubaliano yao.

Tanbihi