Amechaguliwa kuwa mbunge wa IrambaMagharibi mwaka 2010 akarudishwa bungeni kwa miaka 2015 – 2020. [1] Mwaka 2015 alikuwa makamu wa waziri ya fedha.
Baada ya uchaguzi wa 2015 aliteuliwa kuwa waziri wa kilimo, ila mwaka 2016 alibadilishwa kuwa waziri wa mambo ya ndani.
Mwaka 2018 aliondolewa katika nafasi hiyo na raisJohn Magufuli aliyetaja kasoro katika wizara yake kama vile ulaji rushwa, matumizi mabaya ya fedha na kuongezeka kwa ajalibarabarani ilhali mhusika haonekani[2]. Rais alitaja mkataba wa Lugumi ambako polisi ilipata hasara ya Tshbilioni 30, kashfa ya mkataba kwa vifaa vibovu kwenye idara ya NIDA, uigizaji wa magari na malori 700 kwa polisi, mkataba usio halali kwa sare za polisi. Pamoja na hayo watazamaji wengine waliuliza kama jinsi Nchemba alivyojaribu kutafuta mapatano na kanisa la KKKT baada ya barua ya maaskofu ya Pasaka2018 ilijenga wasiwasi wa rais dhidi yake [3].
Katika Februari 2019 Nchemba aliumia katika ajali ambako gari lake liligonga pundamilia wawili barabarani[4]