Kadiri ya Injili ya Yohane, Pilato mwenyewe alisisitiza kwamba, katika maandishi yaliyotakiwa kuwajulisha watu sababu ya adhabu hiyo, iwekwe wazi kwamba Yesu aliuawa kama mfalme wa Wayahudi, ingawa neno hilo lilichukiza viongozi wa taifa.
Maneno ya ilani hiyo yaliandikwa katika lughatatu:
Kilatini: Iesus Nazarenus Rex Iudeorum, kifupi INRI,
Kigiriki: Ἰησοῦς ὁ Ναζωραῖος ὁ Bασιλεὺς τῶν Ἰουδαίω. Kutokana na herufi hizo, Wagiriki wanaandika INBI.
Yesu alipokufa, nafsi yake ya Kimungu iliendelea kushikamana na roho na mwili vilivyotengana: kwa hiyo mwili wake uliozikwa haukuweza kuoza kaburini; roho yake ilishukia kuzimu kuwatoa waadilifu waliomtangulia awaingize pamoja naye mbinguni. “Mwili wake aliuawa, bali roho yake akahuishwa, ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri” (1Pet 3:19). “Roho yake haikuachwa kuzimu, wala mwili wake haukuona uharibifu” (Mdo 2:31).
Mitazamo tofauti
Tangu kale walitokea watu waliokanusha ukweli wa kifo cha Yesu, hasa waliosema yeye hakuwa na mwili halisi, bali alionekana tu kuwa nao.[10][11].
Waislamu wanashikilia msimamo huo, kwamba Yesu hajafa kwa namna yoyote[12], bali alipalizwa mbinguni.
Tanbihi
↑Christopher M. Tuckett in The Cambridge companion to Jesus edited by Markus N. A. Bockmuehl 2001 Cambridge Univ Press ISBN|978-0-521-79678-1 pp. 123–124
↑Eddy, Paul Rhodes and Gregory A. Boyd (2007). The Jesus Legend: A Case for the Historical Reliability of the Synoptic Jesus Tradition. Baker Academic. uk. 172. ISBN978-0801031144. ...if there is any fact of Jesus' life that has been established by a broad consensus, it is the fact of Jesus' crucifixion.
↑Powell, Mark A. Introducing the New Testament. Baker Academic, (2009). ISBN 978-0-8010-2868-7
↑And [for] their saying, "Indeed, we have killed the Messiah, Jesus the son of Mary, the messenger of Allah." And they did not kill him, nor did they crucify him; but rather, it was made to appear to them so. And indeed, those who differ over it are in doubt about it. They have no knowledge of it except the following of assumption. And they did not kill him, for certain. Rather, Allah raised him to Himself. And ever is Allah Exalted in Might and Wise. Quran 4:157–158
Marejeo
Brox, Norbert (1984). "'Doketismus' – eine Problemanzeige". Zeitschrift für Kirchengeschichte. 95. Kohlhammer Verlag: 301–314. ISSN0044-2925.
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kifo cha Yesu kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.